Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:06

IGAD imefanya mkutano wa dharura kuhusu hali iliyopo Sudan Kusini


Kiongozi wa upinzani Sudan Kusini, Riek Machar
Kiongozi wa upinzani Sudan Kusini, Riek Machar

Hatua hii inafuatia mapigano yaliyozuka mwishoni mwa wiki baina ya makundi ya mrengo wa jeshi wa chama cha Makamu Rais wa kwanza Riek Machar, ikiripotiwa kuwepo na watu waliopata majeraha makubwa

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi wanachama wa mamlaka ya kieneo ya serikali na maendeleo (IGAD) wamefanya mkutano wa dharura hii leo, kufuatia mgawanyiko mkubwa uliotokea, ndani ya chama cha SPLA-IO cha Sudan Kusini, huku Washirika wa Riek Machar wakiendelea kulaani majenerali waliotangaza kuondolewa kwake madarakani.

Mawaziri hao kutoka nchi jirani na sudan kusini wamefanya mkutano huo kwa njia ya mtandao kujadili mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo wa hivi karibuni. Hii inafuatia mapigano yaliyozuka mwishoni mwa wiki baina ya makundi ya mrengo wa jeshi wa chama cha Makamu Rais wa kwanza Riek Machar, ikiripotiwa kuwepo na watu waliopata majeraha makubwa.

Kundi la majenerali ndani ya chama cha Machar, cha “Sudan People’s Liberation Movement In Opposition” (SPLM-IO) wiki iliyopita walisema nafasi yake ilichukuliwa na Simon Gatwech Dual kama kiongozi wa mpito wa chama hicho.

Mkutano wa IGAD Uliitishwa na waziri wa mambo ya nje ya sudan kusini, Marian Alsadig al-Mahdi kwa lengo la kusaidia kuokoa mkataba dhaifu wa amani uliotiwa saini mwaka 2018. IGAD imesema hali ya sudan kusini inahitaji uwajibikaji wa haraka. Mapigano baina ya makundi mawili ndani ya SPLM-IO mwishoni mwa wiki yamesababisha vifo vya wanajeshi 34 kutoka pande zote, hiyo ni kwa majibu wa vyanzo mbalimbali vya habari.

Kulingana na msemaji wa Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar kiasi cha wanajeshi 27 kutoka kikundi cha Gatwech waliuawa wakati wa mapigano hayo ya mwishoni mwa wiki.

XS
SM
MD
LG