Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 19:30

Makamishna wa IEBC wakubali kuondoka mamlakani


Raila Odinga kiongozi wa upinzani wa CORD akiwahutubia wafuasi wake katika maandamano ya kuwaping maafisa wa IEBC, Kenya.
Raila Odinga kiongozi wa upinzani wa CORD akiwahutubia wafuasi wake katika maandamano ya kuwaping maafisa wa IEBC, Kenya.

Mwaka mmoja na siku nne kabla ya uchaguzi mkuu nchini Kenya kuitishwa, hatimaye Makamishna wote 9 wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo (IEBC) wameamua kuondoka afisini kwa hiari mradi tu walipwe malimbikizo ya mishahara na marupurupu na shutuma dhidi yao kutochukua mkondo wa kisheria.

Hatua hii inatokana na maandamano ya upinzani nchini Kenya pamoja na shutuma za makundi ya kijamii yaliyoonekana kuishrutisha Tume ya IEBC kung’atuka madarakani. Upinzani unaongozwa na vinara wa CORD wakiwalaumu makamishna wa Tume hiyo kung'ang'ania madaraka, kutoonyesha usawa na kukosa maadili pamoja na kutokuwa huru katika maamuzi yake.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:35 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Muda mfupi baadaye rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wakaamua kuweka kando tofauti zao na kuunda kamati maalum ya bunge ya wanachama 14, saba kutoka kila upande wakiongozwa na maseneta James Orengo na Kiraitu Murungi kusikiliza maoni ya wakenya na kupata suluhu ya kudumu katika mgogoro huo.

Hata hivyo katika siku yake ya pili wiki hii mbele ya kamati hiyo ya bunge, makamishna hao 9 walionekana kusalimu amri. Liwalo na liwe, Kenya ni muhimu kuliko mtu yeyote awaye.

Akiwasilisha ombi hilo mbele ya Tume hiyo inayoongozwa na Orengo na Murungi, mwenyekiti wa tume hiyo, Isaak Hassan, alisema watang’atuka afisini mradi mishahara yao pamoja na marupurupu wanayostahili kulipwa hadi Novemba mwaka ujao yalipwe kwa njia ya masikizano.

Baada ya kila Upande kuwasilisha mapendekezo yake mbele ya kamati hiyo Jumanne, leo Jumatano ilikuwa zamu ya Makamishna hao 9 kila mmoja akielezea msimamo wake kuhusu tuhuma zinazowakabili huku kamishna Yusuf Nzibo akitilia mkazo kauli zao.

Sasa tume hiyo inapotarajiwa kuondoka afisini kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao, mfumo wa kuondoka kwao ndio unaosalia kukubaliwa huku kamati hiyo pia ikitarajiwa kupendekeza baadhi ya mageuzi yanayofaa kufanyiwa tume itakayokabidhiwa jukumu la kusimamia uchaguzi mwaka ujao.

XS
SM
MD
LG