Mkurugenzi wa CIA huko Marekani, John Brennan, anasema idara yake haitatumia adhabu ya kumwagia mtu maji dhidi ya mfungwa, hata kama rais ajaye anaagiza aina kama hiyo ya kufanya mahojiano yanayohusiana na ugaidi.
"Bila shaka sitakubali tena kwa ofisa yeyote wa CIA kutumia mbinu za kuzamisha mfungwa kwenye maji" Brennan alisema katika mahojiano na televisheni ya NBC nchini Marekani, sehemu ya mahojiano ambayo yalirushwa jana Jumapili.