Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 14:56

Idadi ya wazungu yashuka Marekani


Watu wakitembea kwenye mji wa New York

Marekani inasemekana kuwa na idadi kubwa ya watu wenye rangi tofauti wakati idadi ya wazungu ikiwa imepungua katika mwongo mmoja uliyopita

Hilo limejitokeza kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani kupitia sensa mpya ya iliyofanyika mwaka jana.

Idara ya sensa Alhamisi imesema hesabu yake ilionyesha kwamba kulikuwa watu millioni 331.4 wanaoishi Marekani ,likiwa ongezeko la asilimia 7.4 tangu mwaka wa 2010.

Lakini taswira ya taifa kulingana na rangi na kabila ilibadilika, watu wamekuwa wakihamia mara kwa mara kwenye miji mikuu, mara nyingi kwenye majimbo ya Kusini na Magharibi, na wa Marekani ambao wamekuwa mara nyingi wakiondoka kwenye jamii ndogo, mwishowe idadi yao ilipungua.

Watu wanaotambulika kama wazungu bado ni kundi kubwa la raia wa Marekani, lakini idadi yao ilipungua kwa asilimia 8.6 kuliko mwaka wa 2010.

Kundi kubwa la kufuata la watu wanaotambulika kama wa Hispanic au wa Latino, walikuwa sawa na millioni 62.1 mwaka wa 2020, likiwa kundi la wa Marekani ambalo liliongezeka kwa asilimia 23 katika mwongo mmoja.

Wa Marekani weusi walikuwa takriban millioni 46.9, huku wa wamarekani wenye asili ya Asia wakiwa takriban millioni 24.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG