Watu wengi zaidi walinyongwa katika nchi kadhaa mwaka jana kuliko mwaka wowote ndani ya kiaka 25 iliyopita.
Ripoti iliyotolewa na Amnesty International inaeleza kwamba watu 1,634 walinyongwa mwaka jana wa 2015, ikiwa ni ongezeko la asilimia 54 toka mwaka mmoja nyuma ikiwa ni idadi kubwa ambayo kundi hilo la haki za binadamu ilirekodi toka mwaka 1989.
Idadi hiyo kubwa ilitoka katika nchi za Iran, Pakistan, na Saudi Arabia nchi ambazo zilitekeleza adhabu ya kifo ikiwa ni karibu asilimia 90 ya matukio yote ya unyongaji.