Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 18:38

Idadi ya watu waliozidi uzito imeongezeka duniani: Wanasayansi wanasema.


Utafiti mpya unaonesha kwamba idadi ya watoto na vijana walionenepa na kua na uzito mkubwa kuliko ilivyokawaida imeongezeka mara kumi kote duniani katika muda wa miaka 40 iliyopita.

Katika moja wapo ya utafiti mkubwa kabisa wa afya na sababu za magonjwa kufanywa hadi hii leo wanasayansi wa shirika la afya duniani-WHO na chuo kikuu cha Imperial cha London walichunguza takwimu za urefu na uzito za karibu watu milioni 130 tangu 1975 ili kuweza kupata kipimo cha uzito wa mwili BMI.

Watafiti wanasema janga hili kubwa la unene linatokana na matangazo ya biashara ya chakula na upangaji sera dhaifu kote dunaini. Ripoti inaeleza kwamba mabadiliko makubwa yametokea katika nchi zenye mapato ya wastani katika kanda kama vile mashariki ya Asia, mashariki ya, Afrika kaskazini na Amerika kusini.

XS
SM
MD
LG