Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 20:11

Idadi ya vifo yaongezeka Nigeria


Polisi na wafanyakazi wa uokozi katika eneo lililotokea ajali ya ndege na kusababisha vifo vya abiria na wafanyakazi wake mjini Lagos

Rubani mmoja wa shirika binafsi la ndege Nigeria anasema suala kuu ni kwamba wahandisi wanatakiwa kupatiwa mafunzo muda wote

Maafisa wa usalama nchini Nigeria wanasema idadi ya vifo kutokana na ajali ya ndege iliyotokea Jumapili mjini Lagos inakadiriwa 157 baada ya maafisa kuthibitisha vifo vya watu wasiopungua wanne waliokuwa ardhini.

Wafanyakazi wa uokozi wamegundua miili isiyopungua 137 kutoka eneo la ajali lakini mvua na upepo mkali zilipunguza juhudi za uokozi hapo Jumanne.

Ndege ya shirika la Dana ilikuwa ikisafiri kutoka Abuja kuelekea Lagos wakati ilipoanguka kwenye jengo moja katika makazi ya watu. Rubani aliripoti kuwepo na tatizo la injini muda mfupi kabla ya ajali kutokea.

Abiria wote 153 na wafanyakazi wa ndege waliuwawa pamoja na idadi ya watu isiyojulikana waliokuwa chini.

Maafisa wa huduma za dharura wanasema waokozi wamepata chombo cha kunasa sauti cha ndege ambacho kitaweza kutoa habari kuweza kujua chanzo cha ajali hiyo.

Ibrahim Mamman rubani wa shirika hilo binafsi la ndege la IRS nchini Nigeria ameiambia Sauti ya Amerika kwamba suala la kusimamia ndege kufanya kazi vizuri limekuwa tatizo la muda.

“Suala kuu ni kwamba wahandisi wanatakiwa kupatiwa mafunzo. Wanahitaji mafunzo na mafunzo na mafunzo muda wote.”

Shirika la ndege la Dana ni kampuni inayofanya safari za ndani linalosimamia ndege kadhaa za aina ya Boeing MD-83 zinazosafiri kwa saa nyingi kati ya Abuja na Lagos.

XS
SM
MD
LG