Licha ya hilo, watu kadhaa bado wanaendelea kuokolewa kutoka kwenye vifusi.
Siku ya Jumatano wanawake wawili walifukuliwa kutoka kwenye kifusi katika mji wa kusini mwa Uturuki, Kahramanmaras, na mama mmoja na watoto wake wawili waliokolewa mjini Antakya, siku tisa baada ya tetemeko kutokea.
Waokoaji wa Antakya walifika saa 228 baada ya tetemeko kutokea shirika la habari la serekali Anadolu liliripoti.
Mamilioni ya watu ambao wamenusurika wanahitaji misaada ya kibinadamu, serekali imesema huku manusura wengi wakiwa hawana mahali pa kuishi katika kipindi hiki chenye baridi kali.
Waokoaji kwa sasa bado wapo wachache na wakiwa mbali kukamilisha zoezi hilo.
Facebook Forum