Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed atatangaza “hali ya kivita” dhidi ya kundi lenye msimamo mkali wa ki-Islam la al-Shabab lililodai kuhusika kufanya shambulizi hilo Waziri Mkuu wa Somalia alisema.
Marekani inatarajiwa kusaidia katika juhudi mpya za mapigano ambazo Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amepanga kuzianzisha Jumamosi, ofisa mmoja wa jeshi la Somalia aliliambia shirika la habari la Associated Press-AP. Ofisa huyo alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu alikuwa hajapewa mamlaka ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Wakati huo huo msemaji wa jeshi la Somalia Kapteni Abdullahi Iman alisema mapigano yanayojumuisha maelfu ya wanajeshi yatajaribu kuwafurumusha wapiganaji wa kundi la al-Shabaab nje ya ngome zao katika maeneo ya Lower Shabelle na Middle Shabelle mahala ambako yanatokea mashambulizi mengi yanayosababisha vifo kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na kwenye vituo vya jeshi la Somalia na Umoja wa Afrika.