Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 05:39

Idadi ya vifo Italia yafikia 247.


Maafisa wa Italia wamesema idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi la Jumatano imeongezeka na kufikia 247.

Idara ya kulinda raia ya Italia imetangaza idadi mpya Jumatano jioni kutoka idadi ya mwanzo ya watu 124.

Waokozi wanaendelea kutafuta waathirika mpaka usiku ambao wamefukiwa na vifusi.

Mapama Jumatano, waziri mkuu, Matteo Renzi alisafiri kwa helkopta kwenda maeneo yaliyoathirika na kuwafariji waokozi wa kujitolea.

Renzi pia aliongea na waziri wa miundombinu na mkuu wa idara ya uliznzi wa raia.

Tetemeko la ardhi lilipiga eneo moja nchini humo majira ya saa tisa na nusu alfajiri kwa saa za huko na kusababisha uharibifu mkubwa katika miji mitatu karibu na kiini cha tetemeko.

Watoto ni miongoni mwa waliopoteza maisha.

XS
SM
MD
LG