Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 22, 2025 Local time: 06:01

Idadi ya vifo imeongezeka kutokana na mafuriko nchini Afghanistan


Mafuriko yanayoendelea nchini Afghanistan
Mafuriko yanayoendelea nchini Afghanistan

Nyumba zaidi ya 2,600 zimeharibiwa katika eneo lilipotokea mafuriko kufuatia mvua kubwa za msimu.

Maafisa wa Afghanistan wamesema idadi ya vifo kutokana na mafuriko ya Ijumaa katika jimbo la Baghlan kaskazini mwa nchi hiyo imeongezeka na kufikia 315, huku zaidi ya watu 1,600 walijeruhiwa.

Wizara inayohusika na wakimbizi ilitangaza vifo vya hivi karibuni kupitia mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter. Imesema zaidi ya nyumba 2,600 zimeharibiwa kabisa au kwa sehemu, katika jimbo hilo tangu janga lilipotokea kufuatia mvua kubwa za msimu. Wizara hiyo imesisitiza kuwa inaripoti tathmini ya awali kutoka ofisi yake ya Baghlan, ikisema hasara ya kifedha na kibinadamu inaweza kuongezeka.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema Jumapili kuwa maeneo mengi yaliyoathirika katika jimbo hilo hayafikiki kwa malori, na inatumia kila njia mbadala, ikijumuisha punda, ili kuwapatia chakula waathirika ambao walipoteza kila kitu.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilikubaliana na hasara iliyoripotiwa na mamlaka ya Taliban ya Afghanistan, ikisema idadi ya vifo imevuka 300 na kwamba idadi hiyo inatarajia kuongezeka. Shirika hilo limesema mafuriko hayo yameharibu zaidi ya nyumba 2,000.

Forum

XS
SM
MD
LG