Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 05:06

Euro 2016: Iceland yaishangaza Uingereza, Spain nje


Timu ya taifa ya Iceland.
Timu ya taifa ya Iceland.

Raundi ya 16 ya michuano ya kandanda ya kombe la Euro 2016 imeendelea kuleta matokea ya kushangaza huku timu kama Iceland ikiitoa Uingereza katika mashindano hayo kwa ushindi wa 2-1, mabingwa wa zamani Spain wakijikuta nje ya mashindano baada ya kichapo cha bao 2-0 katika mikono ya Italia katika mechi za Jumatatu.

Kwa matokeo hayo mechi za robo fainali tayari zimepangika kuanzia Alhamisi Juni 30 ambapo Poland itachuana na Ureno, Wales itagongana na Ubelgiji Ijumaa Julai 1, na siku ya Jumamosi ni mechi ambayo wengi walitazamia kuona katika fainali kati ya mabingwa wa dunia Ujerumani na Italia. Robo fainali nyingine itakuwa Jumapili Julai tatu kati ya Ufaransa na Iceland.

Nusu fainali zitakuwa Julai 6 na Julai 7 wakati fainali itakuwa Julai 10.

Ushindi wa Iceland dhidi ya Uingereza ulikuwa wa kushtua sana kwani Iceland ni timu ambayo haina uzoefu katika mashindao ya kimataifa. Uingereza walianza vizuri kwa kupata bao la penalty lililofungwa na nyota wa Uingereza Wayne Rooney lakini dakika 18 baadaye Iceland walikuwa tayari wamerudisha goli hilo na kupata bao la pili.

Uingereza kwa mara nyingine inajikuta ikiondoka katika mashindano ya kimataifa licha ya kuwa timu yenye uzoefu mkubwa na nyumbani kwa ligi maarufu kuliko zote ulimwenguni.

XS
SM
MD
LG