Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 07:50

ICC yatoa hati ya kukamatwa Gadhafi.


Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu Luis Moreno-Ocampo .

Mwendesha mashitaka anasema Bw.Gadhafi na serikali yake walifanya mashambulizi dhidi ya raia wakati wa msako dhidi ya waasi waliotaka Bw. Gadhafi kuondolewa madarakani .

Majaji katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC wametoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi na wasaidizi wake wawili waaminifu.

Uamuzi huo umekuja baada ya mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu Luis Moreno Ocampo kuomba hati hizo zitolewe dhidi ya Gadhafi na mtoto wake Seif al Islam na mkuu wa shirika la ujasusi Abdullah al Senussi.

Moreno Ocampo anasema Bw.Gadhafi na serikali yake walifanya mashambulizi dhidi ya raia na kuamuru walenga shabaha kupiga risasi raia walipokuwa wakitoka misikitini wakati wa msako dhidi ya waasi waliotaka Bw. Gadhafi kuondolewa madarakani .

Jaji anayesimamia kesi hiyo Sanji Monageng amesema kuna sababu za kuridhisha kuamini kwamba kiongozi wa Libya na mwanae wanawajibika kiuhalifu kwa mauaji na utesaji wa raia.

Serikali ya Gadhafi inakanusha kulenga raia na badala yake inailaumu NATO kwa kufanya hivyo kwenye mashambulizi ya anga ya kuunga mkono waasi wa Libya.

XS
SM
MD
LG