Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 18, 2025 Local time: 01:51

ICC yatafuta waranti kumkamata Ntaganda


Bosco Ntaganda, anahusika na uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita nchini DRC
Bosco Ntaganda, anahusika na uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita nchini DRC

ICC pia inataka kukamatwa kwa mbabe wa pili wa kivita Sylvestre Mudacumura

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC anasema anatafuta waraka za kukamatwa kwa wababe wawili wa kivita wanaohusika na uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC.

Bosco Ntaganda, anayejulikana pia kama “The Terminator” anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu huko The Hague, tangu mwaka 2006, kwa kutumia watoto kama wanajeshi katika mkoa wa Ituri. Watoto hao walitumiwa kupigana katika kundi la wanamgambo lililoongozwa na Thomas Lubanga, lijulikanalo kama Union of Congolese Patriots- UPC.

Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Luis Moreno Ocampo, aliwaambia waandishi habari Jumatatu kwamba mashtaka yaliyopelekea kuhukumiwa kwa Lubanga, ya kutumia watoto kama wanajeshi ndiyo yaliyopelekea kuibuka kwa ushahidi mpya unaomshirikisha Ntaganda kwa uhalifu huu. Bwana Ocampo anataka kupanua mashtaka na kutoa waraka wa kukamatwa kwake kufuatia tuhuma hizo.

Ocampo anatuhumu kuwa wakati wa mashambulizi yaliyofanywa mwaka 2002 na 2003 kundi la UPC lilizingira miji na vijiji vya kabila la Lendu na kabila nyingine pamoja na kuwapiga risasi na kulenga kuwaangamiza watu wa kabila fulani.

Mbabe wa kivita wa pili ambaye mahakama ya The Hague inataka akamatwe na kufunguliwa mashtaka ni Sylvestre Mudacumura, ambaye ni kamanda mkuu wa kundi la wanamgambo wa kihutu la FDLR.

XS
SM
MD
LG