Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:27

ICC yamhukumu Lubanga miaka 14 jela


 Thomas Lubanga (katikati) akisubiri hukumu yake katika mahakama ya ICC huko the Hague.
Thomas Lubanga (katikati) akisubiri hukumu yake katika mahakama ya ICC huko the Hague.

Kifungo chake kitaanza kuhesabiwa tangu 2006 alipotiwa kizuizini na mahakama ya ICC

Mahakama ya uhalifu ya kimataifa - ICC - imempa kifungo cha miaka 14 jela kiongozi wa waasi wa zamani wa Congo, Thomas Lubanga, baada ya kukutwa na hatia ya kutumia watoto katika mapigano.

Mahakama hiyo mjini the Hague ilitangaza hukumu hiyo Jumanne, ikisema Lubanga alikuwa mtu mwenye elimu ambaye alistahili ubaya ya uhalifu wake. Lubanga alikutwa na hatia mwezi March kwa kuandikisha na kutumia watoto kama wanapiganaji wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mashariki mwa Congo kati ya 2002 na 2003.

Lubanga ni mtu wa kwanza kukutwa na hatia na kupewa kifungo na mahakama ya ICC. Mahakama hiyo imesema kifungo chake kitaanza kuhesabiwa tangu mwaka 2006 alipotiwa kizuizini na ICC.

XS
SM
MD
LG