Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:09

ICC yamfutia mashtaka Muthaura


Francis Muthaura, alikuwa katibu wa baraza la mawaziri nchini Kenya
Francis Muthaura, alikuwa katibu wa baraza la mawaziri nchini Kenya
Mwendesha mashtaka mkuu kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC amefuta mashtaka dhidi ya Mkenya mmoja maarufu aliyeshutumiwa kusaidia kupanga ghasia za baada ya uchaguzi mkuu Kenya mwanzoni mwa mwaka 2008.

Fatou bensouda alisema Jumatatu kuwa anafuta mashtaka dhidi ya Francis Muthaura aliyekuwa katibu wa baraza la mawaziri nchini Kenya na pia mshukiwa mwenza katika kesi ya Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Bensouda alisema hakukuwa na sababu inayoaminika Muthaura atakutwa na hatia katika kesi.
Alisema shahidi muhimu katika kesi alifuta baadhi ya ushahidi wake na alikubali kupokea hongo huku mashahidi wengine wamekufa au wanaogopa kutoa ushahidi. Pia alisema serikali ya Kenya ilishindwa kutoa ushahidi muhimu.

Bensouda alisisitiza uamuzi wa kufuta mashtaka dhidi ya Muthaura hautaathiri kesi nyingine. Bwana Kenyatta na wakenya wawili wengine, ikiwa ni pamoja na makamu rais-mteule, William Ruto, bado wanakabiliwa na mashtaka ya kusaidia kupanga ghasia za kikabila mwanzoni mwa mwaka 2008 ambazo ziliuwa zaidi ya watu 1,100.

Waendesha mashtaka wanasema Rais mteule anawajibika kwa uhalifu dhidi ya kibinadamu ikiwemo mauaji, ubakaji na watu kukimbia makazi yao.

Kesi ya bwana Kenyatta kwenye mahakama ya ICC imepangwa kuanza mwezi Julai.
XS
SM
MD
LG