Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:07

ICC yakataa kuachiwa huru kwa Lubanga

Thomas Lubanga, mshukiwa wa uhalifu wa kivita huko DRC.
Thomas Lubanga, mshukiwa wa uhalifu wa kivita huko DRC.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC – imeamua kwamba mshukiwa wa uhalifu wa kivita kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Thomas Lubanga, hawezi kuachiwa huru na kwamba kesi yake lazima ianze tena.

Mahakama ilitoa uamuzi huo Ijumaa huko The Hague kupinga uamuzi wa awali wa jaji mmoja wa kufuta kesi ya Lubanga na kuamuru aachiwe huru. Afisa mmoja wa haki za binadamu aliusifia uamuzi wa mahakama wa kutaka kesi ya Lubanga isikilizwe tena. Geraldine Mattioli alisema uamuzi huo utawaruhusu waathirika kusikia kama Lubanga ana hatia au la, katika mashtaka hayo.

ICC iliahirisha uamuzi wa mahakama wa mwezi Julai baada ya kusema haitawezekana kupatikana suluhisho la haki kwa Lubanga, hadi waendesha mashtaka watakapotoa jina la mtu anayewezesha mawasiliano kati yao na watu wanaoweza kuwa mashahidi wa kesi hiyo.Waendesha mashtaka walikata rufaa kuhusiana na suala hilo wakisema haitakuwa salama kama watatoa jina na kumtaja mtu huyo.

Lubanga anashtakiwa kwa uhalifu wa kivita akiwatumia watoto kama wanajeshi kupambana katika kundi lake la Union of Congolese Patriots, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka mitano huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambavyo viliisha mwaka 2003. Lubanga alikamatwa mwaka 2006 na amekana makosa.

XS
SM
MD
LG