Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 01:55

ICC kutoa hati za kukamatwa Warussia wanaohusishwa na vita vya Ukraine


Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC)

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) inatarajiwa kutafuta hati za kuwakamata raia wa Russia wanaohusishwa na mzozo wa Ukraine siku za karibuni, chanzo kinachofahamu suala hilo kimesema Jumatatu.

Mwendesha mashtaka wa ICC anatarajiwa kumuomba jaji kabla ya kesi hiyo kuanza ili aadhinishe kutolewa kwa hati hizo za kukamatwa Warussia kadhaa kwa kuwateka nyara watoto kutoka Ukraine na kuwapeleka Russia na kulenga majengo ya raia nchini Ukraine, chanzo hicho kimesema kwa sharti la kutotajwa jina.

Haikufahamika wazi ni watu gani wa Russia ambao ICC inatafuta hati za kuwakamata na lini hati hizo zitatolewa.

Mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan alianzisha uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari nchini Ukraine mwaka mmoja uliopita.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG