Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:41

ICC kufanya uchunguzi Ivory Coast


Wakimbizi wa ghasia za baada ya uchaguzi Ivory Coast wakiwa wamebeba maiti na kuingiza kwenye kambi ya muda iliyokuwa kwenye eneo la kanisa katoliki.
Wakimbizi wa ghasia za baada ya uchaguzi Ivory Coast wakiwa wamebeba maiti na kuingiza kwenye kambi ya muda iliyokuwa kwenye eneo la kanisa katoliki.

Mahakama ya ICC imesema inaruhusu ombi la Moreno Ocampo kupewa idhiniya kufanya uchunguzi akisema watu wapatao 3000 waliuwawa huko Ivory Coast.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC inasema imewahurusu waendesha mashitaka kuanza uchunguzi katika uwezekano wa kuwepo kwa uhalifu wa kivita huko Ivory Coast.

Mahakama yenye makao makuu yake The Hague ilisema katika taarifa Jumatatu inaruhusu ombi la mwendesha mashitaka Luis Moreno-Ocampo kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi katika taifa hilo la Afrika Magharibi kuanzia Novemba 2010.

Moreno Ocampo aliomba kupewa idhini hiyo mwezi Juni , akisema watu wapatao 3000 waliuwawa katika miezi mitano ya mapigano ya kupigania madaraka kufuatia kuchaguliwa kwa rais Alassane Outtara. Vile vile alisema zaidi ya watu 500 walikamatwa na kushikiliwa kiholela na wengine wapatao 100 waliripotiwa kubakwa.

ICC ilieleza Jumatatu kwamba imemuomba mwendesha mashtaka kuwasilisha katika kipindi cha mwezi mmoja habari juu uhalifu wowote mwengine muhimu ambao huenda ulitendeka kati ya 2002 na 2010.

XS
SM
MD
LG