Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 14:35

ICC yawaamrisha watuhumiwa wa Kenya kufika mahakamani


Waandamanaji wa Kenya wakitaka kesi za wahusika na ghasia za baada ya uchaguzi kufikishwa mahakamani The Hague.

Majaji wa mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC wamewaamrisha watuhimiwa 6 wa ghasia na mauwaji baada ya uchgauzi mkuu wa Kenya wa 2007, kufika katika mahakama ya The Hague tarehe 7 April.

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC walitoa amri baada ya kuamua kwamba kuna misingi ya kutosha kuwafungulia kesi watuhumiwa 6 wa ghasai na mauwaji ya Januari 2008.

Wachambuzi wengi wa kutetea haki za binadam wamefurahia tangazo hilo. Hassan Omar kamishina wa tume ya taifa ya haki za binadam anasema, wa-Kenya wengi wamefurahi na wameunga mkono uwamuzi huo.

Anasema, “ni jambo ambalo sote tumekuwa tukilingonjea kwa hamu, kwa sababu kwa wa-Kenya wengi, hatua hii ya korti ya kimataifa ni katika zile hatua ambazo huwenda zikakomesha ile hali ya kutohukumiwa watenda maovu dhidi ya ubinadamu”.

Wakili wa waziri wa zamani biashara, William Ruto mmoja kati ya watu sita wanaotuhimiwa, Bw Katwa Kigen anaendelea kukanusha kuhusika kwa mteja wake na anasema hawakutazamia uwamuzi huo.

Amri ya ICC imetolewa Jumanne wakati makamu rais wa Kenya Kalonzo Musyoka amekua anakutana na maafisa wa Umoja wa Mataifa pamoja na katibu mkuu Ban Ki Moon katika juhudi za kuahirisha kesi hizo. Lakini Bw Omar anasema hadhani juhudi hizo zitaweza kufua dafu.

Hata hivyo, wakili wa Bw Ruto anasema licha ya upinzani wao lakini watakwenda huko The Hague kusikiliza mashtaka na kutetea msimamo wao wa kutohusika na mpango wowote wa kuanda ghasia na mauwaji baada ya uchaguzi mkuu.

XS
SM
MD
LG