Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 15:10

Ocampo:Kifo cha Gadhafi kina mashaka


Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Luis Moreno-Ocampo akielezea kifo cha kiongozi wa zamani wa Libya, Moammar Gadhafi

ICC inasema mazingira yaliyopelekea kifo cha kiongozi wa zamani nchini Libya, Moammar Gadhafi yanatia mashaka

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC anasema kuna “wasi wasi mkubwa” kwamba kifo cha kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi kilikuwa ni uhalifu wa vita.
Luis Moreno-Ocampo alitoa matamshi hayo Alhamis kwenye mkutano mfupi wa Umoja wa Mataifa. Moreno-Ocampo alisema ICC, inaihoji serikali ya mpito nchini Libya namna inavyopanga kuchunguza shutuma za uhalifu wa vita, yakiwemo majeshi yote ya mapinduzi.

Luis Moreno-Ocampo alisema “ninafikiri namna ambavyo bwana Gadhafi alivyouwawa kunajenga wasi wasi wa uhalifu wa vita na ninafikiri kuwa hilo ni jambo muhimu sana”.

Gadhafi alikamatwa na kuuwawa mwezi Oktoba katika mazingira ya kutatanisha. Picha za video na mashahidi zinaonesha kuwa alikuwa mzima baada ya kukamatwa, lakini baadae alionekana kuvuja damu mwilini na kupigwa muda mfupi kabla hajafariki.

Viongozi wa baraza la mpito nchini Libya-NTC wamekuwa chini ya shinikizo kali kutoka mataifa ya magharibi wakiwataka kuchunguza mazingira yaliyosababisha kifo cha Gadhafi.

Moreno-Ocampo anasema ICC pia inafanya kazi na NTC juu ya kesi ya mtoto wa kiume wa Gadhafi, Seif al-Islam, pamoja na mkuu wa zamani wa ujasusi nchini Libya, Absullah al-Sanoussi ambapo walikamatwa wote na wanakabiliwa na mashtaka ya kushiriki kwao katika ghasia za kisiasa nchini humo.

Seif Gadhafi anashikiliwa na maafisa wa Libya na NTC inasema itamhukumu katika mahakama ya nchini Libya.

ICC inataka kuhakikisha kuwa serikali ya mpito inauwezo wa kutoa hukumu sawa kwa Seif Gadhafi. Majaji wa ICC wameitaka NTC kuwafahamisha mipango yao kabla ya Januari 10. Majaji wataamua mahali gani Seif Gadhafi atahukumiwa kama serikali ya Libya inajaribu kuipa changamoto mahakama ya ICC.

Kifo cha Gadhafi na kesi ya Seif Gadhafi ni sehemu ya mashtaka yanayotakiwa kusikilizwa na ICC juu ya shutuma za uhalifu wa vita uliofanywa na majeshi yanayomuunga mkono Gadhafi, wapiganaji wa mapinduzi na majeshi ya NATO.

XS
SM
MD
LG