Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:14

Kimbunga Matthew chasababisha maafa Carribean


A vehicle sits next to a house, stranded in the flood waters caused by Hurricane Matthew, in Leogane, Haiti, Oct. 4, 2016.
A vehicle sits next to a house, stranded in the flood waters caused by Hurricane Matthew, in Leogane, Haiti, Oct. 4, 2016.

Kimbunga kulichopewa jina la Matthew siku ya Jumatano kiliripotiwa kusababisha maafa na uharibifu wakati kikipita Haiti na Cuba kuelekea Bahamas.

Kituo cha kitaifa kinayofuatilia kimbunga huko Miami imesema kuwa Matthew ni hatari sana na kudadisi kuwa kuwa kitaendelea kuwa chenye nguvu hadi Alhamisi.

Kimbunga hicho kilipunguza nguvi baada ya kufika Haiti na kufikia kiwango cha 3 kikiwa na upepo wa maili 125 kwa saa lakini kinatarajiwa kuongeza kasi tena kinapoelekea kwenye ufukwe wa Florida.

Takriban watu 9 wameuwawa nchini Haiti na Jamhuri ya Dominica kutokana na kimbunga hicho ambacho ndicho kibaya zaidi kushuhudiwa katika eneo la Caribbean kwa karibu muongo mmoja huku kikitarajiwa kufika kwenye ufukwe wa marekani baadae wiki hii.

Kimbunga Matthew kimeathiri mawasiliano kati ya mji mku wa Haiti Port du Prince na majimbo matatu na kwa kwavivyo kusababisha hali kuwa gumu kwa maafisa wa uokozi kukadiria hasara iliotokea.

XS
SM
MD
LG