Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 18:28

Human Rights Watch yaiomba Uganda kufuta mashtaka yote dhidi ya mwandishi wa vitabu


Mwandishi wa vitabu Kakwenza Rukirabashaija akifika mbele ya mahakama mjini Kampala, kuomba arudhishiwe pasipoti yake. Februari 1, 2022. Picha ya AP.

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch leo Ijumaa limeiomba Uganda kufuta mashtaka yote dhidi ya mwandishi wa vitabu ambaye alikimbilia uhamishoni, na badala yake ifanye uchunguzi juu ya madai kwamba alinyanyaswa akiwa kizuizini.

Shirika hilo linasema kukamatwa kwa Kakwenza Rukirabashaija ni ushahidi wa mwendelezo wa unyanyasaji wa wapinzani katika taifa hilo la Afrika mashariki, kupitia sheria kali za usalama wa mtandaoni.

Rukirabashaija, mwandishi wa vitabu anayetambulika kimataifa alikamatwa mufa mfupi baaada ya Krismasi kutokana na msururu wa maandishi aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii yanayomkosowa rais Museveni na mwanawe mwenye ushawishi Muhoozi Kainerugaba.

Rukirabashaija amesema aliteswa na waliomuhoji wakati wa kizuizi chake cha mwezi mzima katika kesi ambayo imezuwa taharuki ya kimataifa.

Human Rights Watch imesema katika taarifa yake kwamba “Maafisa wanapaswa kufuta mashtaka yote dhidi ya mwandishi huyo bila masharti yoyote na kuhakikisha kwamba maafisa wote wa usalama waliohusika katika mateso yake na kutoweka kwake wanawajibishwa”,.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG