Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 11:52

Hukumu ya kuuwa hadharani yatumika Jumatano kwa mara ya kwanza tangu utawala mpya wa Taliban, Afghanistan


Afisaa wa Taliban wakati wa mauaji ya hadharani ya awali nchini Afghanistan
Afisaa wa Taliban wakati wa mauaji ya hadharani ya awali nchini Afghanistan

Viongozi wa Taliban nchini  Afghanistan Jumatano wametekeleza  hukumu ya kwanza ya kifo  hadharani kwa mwanaume mmoja aliyetuhumiwa kuua, ikiwa mara ya kwanza kutekeleza  sheria kali za kiislamu tangu kuingia madarakani.

Msemaji wa serikali ya Taliban Zabibullah Mujahid amesema kwamba mauaji hayo yamefanyika alfajiri kwenye uwanja wa michezo kwenye jimbo la magharibi la Farah, baadhi ya walioshuhudia wakiwa maafisa wa ngazi ya juu serikalini, wakiwemo naibu waziri mkuu, mawaziri wa mambo ya nje na mambo ya ndani, pamoja na mamia ya raia.

Hukumu ya mtu huyo ilitolewa baada ya kesi yake kusikilizwa kwenye mahakama ya juu pamoja na ya rufaa ambako alikiri kumuua mkazi mmoja wa Farah, kwa kumchoma kisu, huku akimuibia bidhaa zake, amesema Mujahid. Wakati wa hukumu yake, baba wa mtu aliyeuwawa ndiye alimpiga mshukiwa risasi tatu, msemaji huyo ameongeza.

XS
SM
MD
LG