Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 03:06

Hukumu ya Ghailani yazusha mjadala Marekani


Mawakili wa Ahmed Ghailani, Peter Quijano (kulia) and Steve Zissou wakizungumza na waandishi habari baada ya mashtaka yote isipokua moja yalitupiliwa mbali na baraza la mahakimu.

Tangu mwanzo, kesi ya serikali ya marekani dhidi ya Ahmed Ghailani, raia wa Tanzania, ilichukuliwa kua ni mtihani kwa mfumo wa mahakama ya kiraia ya Marekani ikiwa utaweza kuwahukumu wageni wanaoshukiwa kua ni magaidi. Na hivi sasa hukumu imeshatolewa, na kila mtu anachukulia jinsi alivyo ridhika na kesi hiyo.

Miongoni mwa mashtaka 285 aloshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya 1998, baraza la mahakimu lilimpata Ghailani kua na hatia na shitaka moja tu, nalo ni njama ya kuharibu mali ya Marekani.

Wakili wake Peter Quijano alikua na furaha na kumshukuru hakimu na baraza la mahakimu kwa kesi anayosema ilikua ya haki.

Anasema, “hata kabla ya uwamuzi kutolewa alikua na imani na mfumo wa sheria na alikua na imani na kesi zinazosimamiwa na baraza la mahakimu”.

Watu ambao hawakuridhika sana ni wabunge wa Marekani ambao kwa muda mrefu wamepinga nia ya utawala wa Obama kuwafungulia mashtaka watuhumiwa wa ugaidi wanaoshikiliwa katika jela ya Guantanamo Bay, Cuba katika mahakama ya kiraia badala ya koti za kijeshi.

Seneta Joe Liberman, mwenyekiti wa kamati ya usalama wa ndani katika baraza la Senet anasema, “ninadhani hukumu ya Ghailani haitoshitisha kabisa kesi za kiraia kwa wafungwa, bali ina sababisha kuwepo na uwezekao wa kutofanyika nyingi. Kwake yeye anasema wako vitani na watu wanaokamatwa katika vita ni lazima washikiliwe katia mazingira ya kijeshi.

Liberman ameiambia Sauti ya Amerika kwamba, hukumu ya Ghailani haitatanishi tu kesi za siku zijazo bali pia inasababisha lengo la Rais Obama, la kufunga Guantanamo kua gumu kabisa kulifikia.

Kwa upande wake mbunge atakae kua Spika mpya wa Baraza la Wawakilishi kuanzia mwakani, mrepublicna John Boehner hakuficha upinzani wake. Katika taarifa, Boehner amesema, hukumu ya Ghailani ni ushahidi zaidi kwamba, mpango wa kusikiliza kesi za watuhumiwa wa ugaidi katika mahakama ya kiraia ilikua ni kosa tangu siku ya kwanza. Alitoa wito kwa utawala wa Obama kubadili mkondo na kutowaleta wafungwa wa Guantanamo Bay kwenye ardhi ya Marekani na kuwafungulia mashtaka katika korti za kijeshi.

Makundi ya kutetea haki za binadan na haki za kiraia yanachukua msimamo tofauti. Mkurugenzi wa Human Rights Watch mjini Washington, Tom Malinowski, anasema uwamuzi katika kesi ya ghailani unaonesha kwamba mahakimu wa kiraia na baraza la mahakimu wana uwezo kamili wa kuhukumu kwa haki hata ikiwa uwamuzi haujaridhisha kila mtu.

Malinowiski anasema korti ya kijeshi huwenda ingelitoa uwamuzi kama huo ulotolewa katika kesi ya Ghailani katika mahakama ya kiraia.

Akizungumza na waandishi habari msemaji wa White House Robert Gibbs alidokeza kwamba hukumu ya Ghailani ina adhabu kali ya kifungo cha miaka 20 jela bila ya msamaha na kwamba Ghailani hatokua kitisho tena kwa wa Marekani kutokana na hukumu hiyo. Amesema Rais Obama yungali na nia ya kuifunga Guantanamo, hata ikiwa mpango wake wa awali wa kuifunga jela katika kipindi cha mwaka moja tangu kuchukua madaraka umepitwa na muda..

XS
SM
MD
LG