Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 09:45

Huenda Biden akatangaza jaji mwanamke mweusi kujaza nafasi kwenye mahakama ya juu


Prezidan Joe Biden Pale sou envazyon La Risi fe nan Ikren depi Chanm Es Lamezonblanch la, Jedi 24 Fevriye 2022.
Prezidan Joe Biden Pale sou envazyon La Risi fe nan Ikren depi Chanm Es Lamezonblanch la, Jedi 24 Fevriye 2022.

Vyombo vya habari vya Marekani vimesema Alhamisi kwamba rais Joe Biden amefanya maamuzi ya mwisho kuhusu ni nani atakaye teuliwa kujiunga kwenye mahakama ya juu ya Marekani.

Wakati wa kampeni ya 2020, Biden aliahidi kumteua mwanamke wa kwanza mweusi kwenye mahakama hiyo, suala ambalo alirudia tena baada ya jaji Stephen Breyer mwenye umri wa miaka 83 kutangaza mwishoni mwa mwezi Januari kwamba atastaafu karibuni.

Shirika la habari la CNN limesema kwamba Biden amefikia maamuzi yake, taarifa ambazo pia zimedhibitishwa na shirika la habari la CBS,kutoka kwa vyanzo vya kuaminika vinavyohusika kwenye mchakato wa kujaza pengo hilo.

Taaifa zimeongeza kwamba tangazo hilo huenda likafanywa kati ya Ijumaa na Jumatatu kabla ya Biden kutoa hotuba yake ya hali ya taifa. Kufikia sasa, ikulu ya Marekani haijasema lolote kuhusiana na uteuzi huo.

Miongoni mwa majaji wanaokisiwa kuchukua nafasi hiyo ni Ketanji Brown Jackson kutoka mahakama ya serikali, Michelle Childs kutoka mahakama ya South Carolina na Leondra Kruger kutoka mahakama ya juu ya California.

XS
SM
MD
LG