Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:04

Mashambulizi nchini Afghanistan yawakosesha watoto huduma muhimu


Mtoto wa kiafghanistan akitembea kwenye shamba la afyuni katika wilaya ya Zhari katika jimbo la kusini la Kandahar.
Mtoto wa kiafghanistan akitembea kwenye shamba la afyuni katika wilaya ya Zhari katika jimbo la kusini la Kandahar.

Umoja wa Mataifa umeonya leo Jumatatu kwamba ongezeko la mashambulizi pamoja na matumizi mabaya ya majengo ya afya na elimu kunakofanywa na pande zote kwenye mgogoro wa Afghanistan yamepunguza upatikanaji wa huduma za afya, na kuwazuia watoto kupata huduma hizi muhimu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa na Ofisi ya Misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) na idara ya Umoja wa Mataifa ya kuhudumia watoto (UNICEF) zinasema harakati zinazohusiana na ghasia mwaka uliopita ziliuwa wafanyakazi 31 wa afya na wafanyakazi wa sekta ya elimu, pamoja na kuwajeruhi 58 wengine huku watu 115 walitekwa nyara.

Idadi hiyo inapelekea ongezeko la kubwa zaidi ya matukio yaliyonakiliwa mwaka 2014.

XS
SM
MD
LG