Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, HRW limesema kwamba jeshi la Congo limetoa silaha pamoja na kushirikiana na makundi yanayo shukiwa kusababisha ghasia.
Baadhi ya makundi hayo ni FDLR, la wa Hutu kutoka Rwanda lenye makao yake DRC, na ambalo serikali ya Rwanda inachukulia kama tishio, wakati ikidai kuwa linashirikiana na serikali ya Congo.
Ripoti ya HRW imetolewa wakati kukiwa na taharuki kati ya mataifa hayo, huku DRC ikidai kuwa Rwanda inaliunga mkono kundi la M23, la wa Tutsi wa Congo, ambalo limeshika udhibiti wa maeneo kadhaa mashariki mwa Congo.
Hata hivyo Rwanda imekanusha madai hayo. Mtafiti mkuu wa HRW nchini Congo Thomas Fessy amsema kwamba jeshi la Congo limeanza tena mtindo hatari wa kutumia makundi yenye silaha kama washirika wake. Hadi sasa hakuna tamko lolote lililotolewa na jeshi la Congo kufuatia madai hayo.