Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 11:17

Kenya yaombwa ieleze juu ya kutoweka kwa watu


Polisi wa Kenya wakiwa kwenye doria mitaani

Human Rights Watch inaitaka serikali ya Kenya kuelezea taarifa ya watu waliopotea Mount Elgon miaka mitatu iliyopita

Kundi moja la kueteta haki za binadamu linaitaka Kenya kutoa maelezo juu ya watu wasiopungua 300 ambao walipotea miaka mitatu iliyopita wakati wa msako wa dhidi ya wanamgambo katika eneo la magharibi la Mount Elgon nchini Kenya.

Kundi hilo lenye makao yake Marekani linapendekeza kundi huru kuchunguza makaburi mengi pamoja na shtuma za mauaji yanayodaiwa kuwafanywa na majeshi ya ulinzi ya Kenya dhidi ya kundi la wanamgambo wajulikanao kama Sabaot Land Defense Force-SLDF.

Kundi hilo la haki za binadamu lilisema mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC inatakiwa kuingilia kati kuongoza uchunguzi huo ikiwa kama serikali ya Kenya imeshindwa kufanya hivyo.

Katika ripoti yenye kurasa 48 iliyotolewa Alhamis, Human Rights Watch lilisema ukosefu wa uchunguzi thabiti umesababisha jamaa za watu waliopotea kubaki bila msaada wa kisheria na kisaikolojia.
Mwaka 2008 jeshi la Kenya lilianzisha operesheni ya miezi mitano dhidi ya wanamgambo wa SLDF, ambalo lilidai kupambana kutetea ardhi katika eneo lao.

Makundi ya haki za binadamu yanashutumu kundi la SLDF kwa utekaji nyara, unyanyasaji na kuwauwa raia ambao hawakutii maagizo yake. Pia wameyashutumu majeshi ya Kenya kwa kuwafunga takribani wanaume wote katika eneo la Mount Elgon na kuwanyanyasa na kuwauwa wengi wao wakati wa kuwahoji kwenye kambi za kijeshi.

Human Rights Watch-HRW lilisema kati ya mwaka 2006 na kati kati ya mwaka 2008 kundi la SLDF liliuwa kiasi cha watu 750 na majeshi ya ulinzi ya Kenya yaliuwa watu wanaokadiriwa kuwa 270. HRW linasema kundi jingine la zaidi ya wanaume 300 walitoweshwa. Wengi wa waathirika hao walionekana mara ya mwisho kuwa katika mikono ya majeshi ya ulinzi.

HRW lilisema ripoti yake inaangalia taarifa iliyokusanywa wakati wa uchunguzi na mahojiano katika eneo la magharibi mwa Kenya.

XS
SM
MD
LG