Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 15:31

HRW inasema mashambulizi ya jeshi la Burkina Faso yameua raia 60


Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch Alhamisi limelishtumu jeshi la Burkina Faso kuua takriban raia 60 katika mashambulizi ya ndege isiyokuwa na rubani ambayo serikali ilisema ilikuwa inawalenga wanamgambo wa kiislamu.

Human Rights Watch imesema katika ripoti yake kwamba Vifo hivyo vilitokea katika mashambulizi matatu ya ndege isiyokuwa na rubani tangu Agosti, mawili kwenye masoko yenye watu wengi na jingine katika mazishi,.

Kiongozi wa kijeshi Kepteni Ibrahim Traore ambaye aliingia madarakani baada ya mapinduzi ya 2022, amelipa kipaumbele suala la usalama kwa kutumia nguvu kali kukabiliana na mashambulizi ya makundi yenye uhusiana na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na Islamic State.

Human Rights Watch imesema iliwahoji watu kadhaa na mashahidi kati ya mwezi Septemba na Novemba na ilichunguza picha, video na picha za satellite.

“Jeshi la Burkina Faso lilitumia moja ya silaha zake kali katika zana zake kushambulia makundi makubwa ya watu, na kusababisha vifo vya raia wengi kwa kukiuka sheria za vita, kundi hilo lenye makao yake mjini New York limesema katika ripoti.

Forum

XS
SM
MD
LG