Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 16, 2024 Local time: 00:18

Hotuba ya Obama: maoni yatofautiana


Wapiganaji wa upinzani Libya wakipumzika kwenye mstari wa mbele wa mapambano nje ya mji wa Ras Lanouf mashariki ya Tripoli.
Wapiganaji wa upinzani Libya wakipumzika kwenye mstari wa mbele wa mapambano nje ya mji wa Ras Lanouf mashariki ya Tripoli.

Wachambuzi wa kisiasa na wanasiasa wa Marekani wamegawanyika kutokana na maelezo ya Rais Obama ya kushambulia Libya ili kuwalinda wananchi .

Wabunge wa upinzani wa chama cha Republicans hapa Marekani wamegawanyika juu ya hotuba hiyo ya rais Obama. Seneta John McCain aliyekuwa mpinzani wa Obama wakati wa uchaguzi wa rais wa 2008, alipongeza hatua ya rais huko Libya, lakini amesema mkakati wake ni wa kutatanisha na alichelewa kuchukua uamuzi huo.

Msemaji wa spika wa baraza la wawakilishi John Boehner amekosoa hotuba akisema Bw Obama hakufafanua vyema mkakati wa Marekani huko Libya.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, mhadhiri wa chuo kikuu cha Florida Charles Bwenge anasema "ameweza kutumia nafasi hii kuonyesha uwezo wake wa uongozi na kuhusu sera zake za uhusiano wa kimataifa na jinsi atakavyo shughulikia mizozo inayoibuka kama hii ya Libya".

Kwa upande wa wabunge wa chama cha rais cha Democratic, wengi wamekubaliana na hotuba yake, mwenyekiti wa baraza la Senet Harry Reid amesema hotuba imefafanua mwelekeo uliowazi kuhusiana na uhuru wa watu wa Libya.

Dk. Bashiru Ali, wa chuo kikuu cha Dar es Salaam anasema hakuridhika na hatua kwa sababu Obama alipoingia madarakani aliahidi kubadili sera za aliyemtangulia za kutotumia ubabe katika kutanzua migogoro ya kimataifa.

"Sasa watu wengi tumeshangaa vipi ameweza kuingia Libya na kufanya hayo hayo yaliyofanywa na mtangulizi wake, Je haoni kwamba amesaliti nia na ahadi aliyotoa kwa Marekani na dunia nzima."

XS
SM
MD
LG