Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 16:07

Hotuba ya Obama inatarajiwa kumjenga Clinton


Mgombea urais wa Democratic, Hillary Clinton, July 26, 2016.

Wa-democratic wanamatumaini kwamba Rais Barack Obama atamsaidia mgombea urais Hillary Clinton kuleta nguvu ndani ya chama wakati anapotoa hotuba yake Jumatano kwenye mkutano mkuu wa Democratic.

Bwana Obama ni maarufu sana miongoni mwa wa-Democratic, lakini bado anapingwa nchini Marekani huku kukiwa na kiasi cha mmarekani mmoja kati ya wawili wakiidhinisha utendaji kazi wake, hata hivyo wengi hawafurahishwi na wagombea wote Clinton na mpinzani wake Donald Trump wa Republican, uungaji mkono wa Obama unaonekana kama wa kumsaidia Hillary.

Kwa rais kusaidia kuchaguliwa Clinton kutasaidia kulinda mafanikio yake mengi muhimu akiwa madarakani kama vile kupanua fursa za huduma ya afya na mkataba wa nyuklia na Iran.

XS
SM
MD
LG