Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:32

Trump atoa maneno makali kwa Clinton


Mgombea anayetarajiwa kuteuliwa wa chama cha Republikan hapa Marekani, Donald Trump, Alhamisi usiku alimjibu vikali mgombea anayeongoza wa tikiti ya Demokratik, Hillary Clinton, kufuatia hotuba juu ya sera za kigeni aliyoifanya waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje.

Clinton alimshambulia kwa maneno makali Trump, na kumtaja kama asiye na fikra timamu za kuongoza Marekani huku akisema kazi hiyo, inahitaji ujuzi, uthabiti na uwajibikaji mkubwa.

Lakini Trump alimjibu kwa kusema kuwa fikra zake ni timamu kuliko za Clinton. Trump, aliyekuwa akizungumza mjini San Jose, California, alisema Hilary ni mdanganyifu na kwamba hakusema ukweli kuhusu sera ambazo Trump amekuwa akisema angezingatia endapo atachaguliwa kuwa rais.

Kabla ya Trump kutoa hotuba yake, Clinton alisisitiza kwamba ana uzoefu mwingi alioupata kama mke wa rais, kama seneta na kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani, na kuongeza kuwa angetoa mwelekeo dhabiti wa kidiplomasia ambao unahitajika na Marekani.

XS
SM
MD
LG