Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:08

Hoteli ya Muna yashambuliwa kwa bomu huko Somalia.


Wasomali wakiangalia gari lililotumika kwenye mlipuko wa bomu katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Wasomali wakiangalia gari lililotumika kwenye mlipuko wa bomu katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Mlipua mabomu wa kujitoa muhanga ashambulia hoteli huko Mogadishu nan kuuwa watu 9.

Mshukiwa wa bomu la kujitoa muhanga ameshambulia hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kuuwa watu 9 na kujeruhi wengine wengi.

Mshambuliaji huyo alishambulia hoteli ya Muna , ambayo ipo karibu na jumba la rais na inajulikana kama nyumba na makutano kwa wabunge wa Somalia.

Maafisa wanasema mlipuaji huyo alitega bomu kwenye gari lililojaa milipuko jumatano kwenye mgahawa nje ya hoteli ambapo watu wengi walikuwa wamekaa.

Hakukuwa na waliodai kuhusika mara baada ya mlipuko huo. Wanamgambo walishambulia hoteli hiyo hiyo pia mwaka 2010.

XS
SM
MD
LG