Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:05

Msaada watolewa kupambana na homa ya manjano


Luanda, Angola
Luanda, Angola

Shirika la Msaada Mwekundu leo Jumatano limetoa wito wa msaada wa dharura wa dola milioni 1.4 ili kukabiliana na kuenea kwa homa ya manjano nchini Angola ukiwa mlipuko mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30.

Kufikia sasa, zaidi kidogo ya dosi milioni 15 za homa ya manjano zimepelekwa Angola pamoja na nchi jirani ya DRC lakini uhaba wa fedha na ugumu wa kutengeneza chanjo vimepelekea upungufu huo.

Homa ya manjano maarufu 'Yellow Fever' ni ugonjwa unaoenezwa na mbu. Mbu wanaoeneza homa ya manjano ndio wanaoeneza Zika, homa ya Dengue pamoja na Chikungunya.

Homa ya manjano mara nyingi haijioneshi dalili na wengi walioambukizwa dalili hazijitokezi, hata hivyo takriban asilimia 15 ya wagonjwa huathiriwa vibaya huku aslimia 50 wakifa kutokana na maradhi hayo wanapokosa matibabu.

XS
SM
MD
LG