Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:12

Homa ya ini inaweza kuua watu wengi zaidi kuliko HIV, malaria na kifua kikuu ifikapo mwaka 2040-Mashirika ya afya


Nembo ya WHO nje ya jengo la shirika hilo la afya duniani mjini Geneva.
Nembo ya WHO nje ya jengo la shirika hilo la afya duniani mjini Geneva.

Mashirika ya afya yanaonya kwamba homa ya ini inaweza kuua watu wengi zaidi ifikapo mwaka wa 2040 kuliko HIV, kifua kikuu, na malaria kwa pamoja ikiwa ugonjwa huo utaendelea kupuuzwa na kutofadhiliwa vya kutosha.

Shirika la afya duniani (WHO) linaripoti kila mwaka kwamba homa ya ini, inaathiri zaidi ya watu milioni 350 ulimwenguni na kuua zaidi ya watu milioni 1. Asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa na kuuawa na ugonjwa huo ni kutoka nchi zenye pato la chini na la kati.

Licha ya tiba ya homa ya ini aina ya C na chanjo dhidi ya homa ya ini aina ya B, watetezi wa ulimwengu usio na ugonjwa huu hatari na unaoodhofisha bado hawajafikia lengo lao.

“Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, tumeshuhudia mafanikio makubwa katika safari hii ya kutokomeza homa ya ini,” amesema Oriel Fernandez, mkurugenzi mkuu wa mpango wa homa ya ini duniani kwenye kituo cha Clinton Health Access Initiative au CHAI.

“Gharama ya jumla ya kuponya mgonjwa ilishuka kwa asilimia 96 kutoka zaidi ya dola 2,500 kwa kila mtu hadi chini ya dola 80 kwa kila mtu aliyeponywa, Oriel amesema.

XS
SM
MD
LG