Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 19:34

Hisia mseto zimeendelea kutolewa kufuatia kujiuzulu kwa Liz Truss


Liz Truss alipowasili Number 10 Downing Street, London, Uingereza Septemba 6, 2022. REUTERS/Phil Noble.
Liz Truss alipowasili Number 10 Downing Street, London, Uingereza Septemba 6, 2022. REUTERS/Phil Noble.

Hisia mseto zimeendelea kutolewa kufuatia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss Alhamisi baada ya siku 44 tu madarakani,.

Hayo yalijiri huku akichochewa na mpango wa kiuchumi uliopelekea soko la fedha kudorora, na kusababisha mtikisiko katika Baraza lake la Mawaziri na kugawanya chama chake tawala cha Conservative.

Akiwa ni waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi katika historia ya Uingereza.

Katika maoni yaliyotolewa kwenye jukwaa mbele ya makazi ya waziri mkuu huko No. 10 Downing Street mjini London, Truss alisema kwamba wakati aliweka maono ya "kodi ya chini,ukuaji wa uchumi," alitambua kuwa hangeweza kutekeleza ilani ambapo alichaguliwa na Chama cha Conservative.

Truss alisema atahudumu hadi mtu mwingine atakapochaguliwa. Graham Brady, mwenyekiti wa baraza maalum la wabunge wa Chama cha Conservative, Kamati ya 1922, aliwaambia waandishi wa habari kwamba uongozi wa chama umeonyesha kuwa unaweza kupiga kura na kuhitimisha uchaguzi mapema Oktoba 28, na ikiwezekana kuwa na waziri mkuu mpya ifikapo Oktoba 31.

Kamati ya 1922 inaundwa na wabunge wa Chama cha Conservative na ina uwezo wa kulazimisha waziri mkuu kutoka ndani ya chama kujiuzulu.

Wachambuzi wanapendekeza aliyekuwa waziri wa fedha Rishi Sunak, ambaye alishindwa na Truss katika kinyang'anyiro cha mwisho cha uongozi mwezi Agosti, ndiye anayeongoza katika kuchukua nafasi yake.

Wakati huo huo, rais wa Marekani Joe Biden siku ya Alhamisi alimtaja Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss, ambaye anajiuzulu baada ya wiki sita tu za uongozi wake wenye misukosuko, mshirika mzuri katika kuiunga mkono Ukraine kujilinda dhidi ya uvamizi wa Russia. Lakini alikataa kueleza juu ya kujiuzulu kwake.

“Hilo ni lake yeye kuamua," Biden aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu muda mfupi kabla ya kupanda helikopta ya rais Marine One akielekea Pennsylvania.

"Lakini angalia, alikuwa mshirika mzuri wa juu ya masuala ya Russia na Ukraine, na Waingereza watatatua shida zao."aliongeza.

Biden alitupilia mbali athari zozote zinazoweza kutokea kutokana na msukosuko wa kisiasa wa mshirika mkongwe zaidi wa Marekani."Sidhani kama ni mabaya kiasi hicho" alisema.

XS
SM
MD
LG