Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 21:25

Hisa Zaanguka Masoko ya Ulaya


Kampuni ya Udalali, Shanghai, China
Kampuni ya Udalali, Shanghai, China

Masoko makuu ya fedha ya Ulaya yalianguka vibaya mapema leo alhamisi baada ya China kusimamisha kwa muda biashara ya kuuza hisa kutokana na hasara ya kuuza kwa bei ya chini .

Anguko la leo la asilimia 7 katika nusu saa ya kwanza ya biashara kwenye soko la Shanghai Composite index ilisababisha idara inayofuatilia masuala ya biashara nchini China kusimamisha biashara kwa siku hii.

Hatua hiyo iliwaudhi wawekezaji kwenye eneo zima na kusababisha masoko mengine ya Asia kushuka na kusababisha kupungua thamani kwa sarafu ya China ya Yuan dhidi ya Dollar ya Marekani.

XS
SM
MD
LG