Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 11, 2024 Local time: 06:00

Hiroshima yaadhimisha miaka 65


Mji wa Hiroshima, Japan waadhimisha miaka 65 tangu shambulizi la bomu la atomic. Nchi za magharibi zashiriki kwa mara ya kwanza.

Mji wa Hiroshima nchini Japan unaadhimisha miaka 65 ya kumbukumbu ya shambulizi la bomu la atomiki. Sherehe za mwaka huu zinatiliwa maanani kwa sababu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon anahudhuria kwa mara ya kwanza ikiwa ni pamoja na wanadiplomasia kutoka mataifa yenye nguvu yaliyoishinda Japan katika vita kuu ya pili ya dunia. Mataifa hayo ni pamoja na Marekani ambayo ilitupa bomu hilo la nyukilia katika mji wa Hiroshima august 6 mwaka 1945 katika siku za mwisho za vita hivyo.

Watu 120,000 waliuawa siku hiyo ama walikufa katika kipindi cha miezi kadha kutokana na athari za mionzi au majeraha. Kabla ya mwaka mwaka huu Marekani imekuwa ikikataa kuhudhuria maadhimisho hayo. Lakini mwaka huu balozi wa Marekani huko Japan John Roos amehudhuria ingawa hakuzungumza katika maadhimisho hayo.

Ubalozi wa Marekani mjini Tokyo ulitoa taarifa iliyosema balozi Roos amehudhuria ili kutoa heshima zake kwa wale ambao waliathirika na shambulizi hilo. Alisema katika taarifa hiyo kuwa Marekani na Japan zilirejesha ushirikiano wao na "kwa faida ya kizazi kijacho lazima tuendelee kushirikiana."

Shirika la habari la Japan, NHK, limeripoti kuwa baadhi ya watu walionusurika kutokana na shambulizi hilo wanasema Marekani imechelewa kubadilisha tabia yake lakini baadhi wamekubali heshima hiyo.

Wajumbe kutoka Uingereza na Ufaransa, nchi ambazo pia zina silaha za nuklia, wamehudhuria maadhimisho hayo kwa mara ya kwanza pia.

XS
SM
MD
LG