Shambulizi kama hilo linalohusisha ndege zisizokuwa na rubani litakuwa la kwanza kutekelezwa na Hezbollah tangu kuanza kwa majibizano ya silaha na Israel ambayo yamekuwa yakiendelea huku Israel ikipambana na kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Jeshi la Israel halijatoa taarifa yoyote kuhusu mashambulizi hayo lakini ving’ora vilisikika kaskazini mwa Israel mara tatu leo Jumatatu huku onyo la kutokea mashambulizi kutoka Lebanon likitolewa.
Israel imesema kwamba imemuua jasusi wa kijeshi wa Hezbollah Ali Hussein Sabra na kwamba wanajeshi wake walitekeleza mashambulizi dhidi ya mfumo wa Hezbollah katika sehemu kadhaa za Qotrani, kusini mwa Lebanon.
Kundi la Hezbollah limesema kwamba mashambulizi yake yametokana na hatua ya Israel kuua mmoja wa wanachama wake katika kijiji cha Zrariyeh, kusini mwa Lebanon. Kundi hilo linaloungwa mkono na Iran pia limesema limetekeleza mashambulizi kuelekea Liman, kaskazini mwa Israel.
Forum