Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 15:03

Maoni mbalimbali yatolewa kuhusu Brexit


Watu wa Uingereza leo wameamua kupitia kura ari yao ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya swala ambalo baadhi ya viongozi wa Ulaya wanasema hatua ya wananchi wa Uingereza ni kosa kubwa.

Chancela wa Ugerumani, Angela Merkel, amesema kuwa hakuna shaka kwamba tukio hilo ni pigo kubwa kwa Ulaya.

Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, pia amesema Uingereza imefanya kosa kubwa kujiondoa kwenye muungano huo ambao ndio soko kubwa zaidi ulimwenguni. Amesema kuwa haamini mataifa mengine yako tayari kufuati njia hiyo hatari.

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, amesema kuwa ana uhakika Uingereza itabaki mshirika wa karibu wa NATO na kwamba itaendelea kutoa uongozi katika shirika hilo lenye uhusiano wa karibu na Umoja wa Ulaya.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema amehuzunishwa na hatua hiyo ingawa lazima uamuzi wa watu wa Uingereza uheshimiwe.

XS
SM
MD
LG