Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 21:11

Hatma ya Ramaphosa madarakani kuamuliwa na chama chake cha ANC


Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa akihutubia kongamano kuu la chama cha African National Congress ANC, mjini Johannesburg, July 29, 2022
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa akihutubia kongamano kuu la chama cha African National Congress ANC, mjini Johannesburg, July 29, 2022

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa anakabiliwa na hali ngumu ya kisiasa kujisafisha kutokana na tuhuma za utakatishaji wa fedha licha ya bunge kumuondolea lawama na kunusurika kura ya kutokuwa naye bungeni.

Sakata hiyo imeharibu sifa ya uongozi ya Ramaphosa, ambaye alipigania haki za watu wa Afrika kusini na kupinga ubaguzi nchini humo, na ambaye amesifiwa kwa kutatua matatizo ya nchi hiyo ambayo imeendelea zaidi Afrika.

Cyril Ramaphosa, mwenye umri wa miaka 70, amesisitiza kwamba hakufanya kosa lolote kutokana na shutuma kwamba alificha kiasi cha dola 580,000 ndani ya kiti katika shamba lake.

Anashutumiwa kwa kukosa kutangaza pesa hizo kwa serikali, na kukosa kuripoti baada ya pesa hizo kuibwa, huku akikosa kujibu maswali namna alivyopata dola hizo za Marekani.

Chama kinachotawala Afrika kusini ANC, kinatarajiwa kupiga kura leo Ijumaa, kuamua iwapo Ramaphosa anastahili kuvuliwa nafasi ya kiongozi wa chama, hatua itakayomlazimisha kujiuzulu.

Marais wawili wa Afrika kusini, waliotawala kabla ya Ramaphosa, walilazimika kujiuzulu baada ya kuondolewa nafasi ya uongozi wa chama kinachotawala cha African national congress ANC kutokana na Sakata zinazohusiana na ufisadi.

XS
SM
MD
LG