Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 17:31

Hatma ya baadaye ya Somalia yajadiliwa.


Mwakilishi wa maalum wa Umoja wa Mataifa Somalia Augustine Mahiga, wa tatu kulia akisamiwa na waziri mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali, wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mogadishu.
Mwakilishi wa maalum wa Umoja wa Mataifa Somalia Augustine Mahiga, wa tatu kulia akisamiwa na waziri mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali, wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mogadishu.

Muda wa kuhudumu wa serikali ya mpito ya Somalia unakamilika mwezi Agosti na mkataba uliofikiwa Garowe unatarajiwa kuleta mabadiliko .

Muda wa kuhudumu kwa serikali ya mpito ya Somalia –TFG unakatika mwezi Agosti mwaka huu. Na kutokana na ugumu uliopo wa kuweza kuandaa uchaguzi mkuu katika mazingira ya machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe viongozi wa Somalia na wale wa kimataifa walikamilisha mkutano Jumamosi kwa makubaliano ya kuunda mpango wa kuteuwa serikali mpya katika muda wa miezi sita ijayo. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia balozi Augustine Mahiga alisema mkataba uliofikiwa katika mji wa Garowe utaleta utawala halali na unaohitajika sana Somalia. Mpango mpya wa kuunda serikali mpya na halali ya Somalia utakuwa na viti 1000 vya bunge ifikapo mwezi Aprili. Wabunge hao watachaguliwa kutoka mashinani na miongoni mwao kutakuwa na wanawake , wazee , viongozi wa kidini wasomi na Wasomali wanaoishi nje ya nchi. Wabunge watakaoteuliwa wanatazamiwa kuanza kazi zao bungeni mwezi mei na watamchagua spika ifikapo Juni na rais mwezi julai. Balozi Mahiga alisema kundi la wanamgambo wa kiislam lenye msimamo wa kadri pia litajumwishwa kwenye mkusanyiko huo wa kisiasa. Idadi ya viti bungeni itapunguzwa kutoka 550 hadi 225. Balozi Mahiga alieleza furaha yake kwamba chini ya makubaliano mapya asili mia 30 ya viti vya bunge vitakuwa vya wanawake na hivyo kuongeza idadi ya uwakilishi wa wanawake katika bunge la Somalia kwa asilimia 12.5. Mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia atakwenda London, ambapo Alhamis wiki hii, serikali ya Uingereza imeandaa kongamano kubwa kujadili hali ya baadaye ya Somalia .

XS
SM
MD
LG