Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 12:57

Hatimaye Mubarak ajiuzulu urais Misri


Wananchi wa Misri wakishangilia kujiuzulu kwa Rais Hosni Mubarak
Wananchi wa Misri wakishangilia kujiuzulu kwa Rais Hosni Mubarak

Rais wa Misri Hosni Mubarak amejiuzulu uongozi wa nchi hiyo baada ya kukaa madarakani kwa miaka 30. Tangazo la kuondoka madarakani kwa kiongozi huyo lilitolewa na Makamu Rais Omar Suleiman ambaye alisema jeshi sasa litachukua uongozi.

Tamko la kujiuzulu kwa Mubarak lilipokewa kwa shangwe kubwa katika uwanja wa Tahrir Square mjini Cairo ambako maandamano yamekuwa yakifanyika kwa siku 18 sasa. Wengi wao walikuwa wanapeperusha bendera za Ethiopia.

Mapema Ijumaa, vyombo vya habari vilikariri maafisa wakisema Bw Mubarak ameondoka mjini Cairo kuelekea katika nyumba yake ya mapumziko katika mji wa Sharm El-Sheikh. Ikulu ya Marekani ilipokea kujiuzulu huko kwa kusema "ni hatua nzuri"

XS
SM
MD
LG