Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:17

Hatimaye Israel na Lebanon zimekubaliana kuhusu mpaka


Mpaka wenye utata kati ya Israel na Lebanon katika picha hii iliyopigwa kutoka Rosh Hanikra, karibu na mpaka wa Lebanese border, kaskazini mwa Israel Oct 27, 2022
Mpaka wenye utata kati ya Israel na Lebanon katika picha hii iliyopigwa kutoka Rosh Hanikra, karibu na mpaka wa Lebanese border, kaskazini mwa Israel Oct 27, 2022

Viongozi wa Israel na Lebanonleo wamesaini makubaliano ya kihistoria yaliyosimamiwa na Marekani ya mpaka wa baharini.

Hatua hiyo ni inafikisha mwisho mgogoro wa kidiplomasia wa miongo kadhaa na kutoa fursa ya kuanza uchimbaji wa mafuta baharini.

Rais wa Lebanon Michel Aoun amesaini barua ya kuidhinisha mkataba huo mjini Baada, na kufuatiwa na waziri mkuu wa Israel Yair Lapid mjini Jerusalem.

Hafla ya kukabidhiana mkataba huo zinatarajiwa kufanyika katika kambi ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ya Naqoura, kwenye mpaka wa Israel na Lebanon.

Lapid amepongeza mkataba huo kama mafanikio makubwa sana huku mjumbe wa Lebanon Elias Bou Saab akisema kwamba ni mwanzo mpya kwa nchi hizo mbili ambazo kimkakati zinakabiliwa na tisho la mapigano.

"Haya ni mafanikio ya kiuchumi. Jana uchimbaji mafuta ulianza katika vitalu vya Karish. Israel itapokea asilimia 17 ya faida kutoka kwenye vitalu vya Qana-Sidon vya Lebanon, na pesa hizo kutumika kujenga uchumi wa taifa, kugharamia sekta za ustawi wa jamii, afya, elimu, na usalama."

Makubaliano hayo yanaondoa uwezekano wa kutokea vita kati ya Israel na kundi la Hezbollah, linaloungwa mkono na Iran, na yanaweza kuisaidia Lebanon kujiondoa katika mgogoro wa kiuchumi.

Baada ya kikao na spika wa bunge la Lebanon Nabih Berri, mjumbe wa Marekani katika mazungumzo kati ya Israel na Lebanon Amos Hochstein, amewaambia waandishi wa habari kwamba wanatarajia nchi hizo mbili kuutekeleza mkataba huo licha ya mabadiliko katika uongozi wake.

XS
SM
MD
LG