Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 04:22

Bashir aomba visa kuhudhuria Umoja wa Mataifa


Rais Bashir akutana na Salva Kiir.

Serikali ya Sudan inatumai kwamba utawala wa Rais Barack Obama utampa hati ya kusafiria Rais Omar Al Bashir ili kuhudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York mwaka huu.

Waziri wa habari Ahmed Bilal alisema kuwa Rais Bashir amealikwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki Moo, kuhudhuria kikao hicho mwezi Septemba. Alisema ni wajibu wa Marekani, ambako ndiko mkutano huo utafanyika, kumpa Rais Bashir visa ya kusafiria.

Waziri huyo alisema kwamba maombi ya kutaka kuja Marekani yaliyofanywa na Bashir mara ya mwisho, yalikataliwa. Aliongeza kuwa kwa sababu sasa rais huyo amealikwa rasmi, ni wajibu wa Marekani kumpa kibali cha kuhudhuria shughuli za Umoja wa Mataifa, na kwamba serikali ya Sudan haioni sababu ya kumkatalia kufanya hivyo.

Bilal alisema hiyo ndiyo sababu Rais Bashir amefanya ombi hilo na kwamba iwapo atakubaliwa, basi atafanya safari hiyo.

Wiki iliyopita, Bashir alihudhuria sherehe za kutawazwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni mjini Kampala. Ujumbe wa Marekani uliondoka kutoka sherehe hiyo baada ya Museveni kusema kwamba mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu, ICC, haina maana yoyote.

Bashir anasakwa na mahakama hiyo kwa shutuma za uhalifu wa kivita katika eneo la Dafur ambako inakadiriwa kwamba watu wapatao 300,000 waliuawa na wengine milioni mbili kufurushwa makwao.

XS
SM
MD
LG