Michele Obama, atamfanyia kampeni Harris katika jimbo la Michigan.
Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump vile vile anatarajiwa kufanya kampeni katika jimbo hilo la Michigan, ambalo ni mojawapo ya majimbo saba yenye ushindani mkali na magumu kutabiri mshindi.
Jimbo la Michigani lina wapiga kura milioni 8.4, na kura za wajumbe 15 kati ya kura za wajumbe 270 ambazo mshindi wa urais anatakiwa kuzipata.
Michigan ni jimbo ambalo wademocrat wana matumaini kwamba Harris tapata ushindi.
Majimbo mengine yenye ushindani na yenye matumaini kwa Wademocrat ni pamoja na Pennsylvania na Wisconsin.
Forum