Amesisitiza kwamba Marekani itaendelea kuhakikisha kwamba usalama wa washirika wake barani Asia unalindwa kutokana na vitisho vinavyoongezeka na uchokozi wa Korea kaskazini.
Ziara ya Harris inajiri wakati Korea kaskazini imekuwa ikifanya mazoezi ya makombora huku kukiwepo wasiwasi kwamba nchi hiyo huenda ikafanyia majaribio silaha za nuclear.
Ametembelea sehemu hiyo ya mpakani baada ya kutembelea wanajeshi na baadhi ya watu wa familia zao katika kambi ya kijeshi ya Bonifas ambapo alisema kwamba alitaka wanajeshi hao watambue namna uongozi wa Marekani unawashukuru kwa kazi wanayofanya.
Harris amefanya mazungumzo na rais wa Korea kusini Yoon Suk Yeol, mjini Seoul, leo alhamisi.