Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:44

Makamu Rais mteule Harris amchagua Jaji Sotomayor kumuapisha


Makamu wa Rais mteule Kamala Harris
Makamu wa Rais mteule Kamala Harris

Makamu wa Rais mteule wa Marekani, Kamala Harris ataapishwa na Jaji wa Mahakama ya Juu Sonia Sotomayor Jumatano.

Tukio hilo linaweka historia ya mwanamke mweusi wa kwanza, kutoka Asia Kusini kuapishwa kuchukua nafasi ya makamu rais na jaji wa kwanza mwenye asili ya Amerika Kusini.

Jaji Sonia Sotomayor
Jaji Sonia Sotomayor

Harris amemchagua Sotomayor kumuapisha, kulingana na mtu anaefahamu namna uamuzi huo ulivyochukuliwa. Pia atatumia Bibilia mbili wakati wa kuapishwa, moja ilikuwa ni ya Thurgood Marshall, Jaji wa kwanza mweusi wa Mahakama ya Juu.

Jaji Thurgood Marshall
Jaji Thurgood Marshall

Kituo cha Televisheni cha ABC ni cha kwanza kutangaza taarifa hiyo kuhusiana na mipango ya kuapishwa Harris.

Harris ameeleza kuvutiwa kwake na wote wawili Sotomayor na Marshall. Yeye na Sotomayor wanauzoefu sawa wa kufanya kazi kama waendesha mashtaka, na kuna wakati alimtaja Marshall – kama alivyo Harris, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Howard – kuwa moja wa “mashujaa wake wakubwa.”

Makamu wa rais mteule amesema katika video iliyowekwa katika mtandao wa Twitter kuwa alikuwa anamuona Marshall kama “moja ya sababu kuu iliomfanya awe mwanasheria,” akimtaja kuwa ni “mpiganaji” katika chumba cha mahakama.

Na hii itakuwa ni mara ya pili kwa Sotomayor kushiriki katika zoezi la kuapisha. Alimuapisha Rais mteule Joe Biden kuwa makamu wa rais mwaka 2013.

XS
SM
MD
LG