Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 02:36

Hamdok aahidi kuendeleza ushirikiano na watetezi wa demokrasia


Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok, ameahidi Jumatano kufanya kazi pamoja na makundi ya kutetea demokrasia kwa mara nyingine, na kuepesha vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe.

Hamdok amesema makundi yaliyofanikisha mapinduzi ya kumuondoa rais wa muda mrefu wa Sudan, Omar al Bashir, mwaka 2019 lazima yashikamane kwa kufanya mazuri kwa Sudan.

Katika hotuba ya televisheni amejaribu kuwahakiishia wananchi wa Sudan kwamba mabadiliko magumu na yenye matarajio makubwa yaliyoanzishwa na serikali yake ya mpito yatabadilisha uchumi.

Saa kadhaa mapema, Jumatano mazungumzo ya amani baina ya serikali na makundi makubwa ya waasi yaliahirishwa ili kutoa nafasi kwa pande zote mbili kupitia mchakato na kutafuta suluhu.

Habari inatokana na vyanzo mbalimbali

XS
SM
MD
LG